Gavana Achani atoa hundi ya karo ya shilingi milioni 14 kwa shule ya Kwale

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amekabidhi hundi ya msaada wa masomo ya shilingi milioni 14 kwa shule ya kitaifa ya Kwale kufadhili wanafunzi 640 waliokuwa wamesalia nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa karo.

Akizungumza katika hafla ya utoaji hundi  Gavana wa Kwale  Fatuma Achani amepongeza hatua ya Serikali ya kitaifa kuruhusu serikali za kaunti kuwasaidia watoto werevu kutoka familia maskini.

Takribani wanafunzi elfu 17 wamepata ufadhili wa masomo katika kaunti ya Kwale tangu kuzinduliwa kwa mradi huo.

Share This Article