Sheila Chepkirui wa Kenya mapema Jumapili amesherehekea siku ya kimataifa ya wanawake kwa njia ya kipekee baada ya kuhifadhi taji la mbio za Nagoya Marathon nchini Japani.
Chepkirui ameziparakasa mbio hizo kwa kuweka rekodi mpya ya mkondo ya saa 2, dakika 21 na sekunde 54.
Nafasi ya pili ilimwendea Sayaka Sato wa Japani kwa saa 2 dakika 21 na sekunde 56, huku Aynalem Desta wa Ethiopia akihitimisha tatu bora kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 37.