Kenya na Norway kuimarisha fursa za biashara na uwekezaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi ashiriki mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Andreas Motzfeldt Kravik nchini India.

Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amesema Kenya na Norway zitaendeleza ushirikiano wao katika maswala ya maendeleo, biashara, amani na usalama.

Akizungumza alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Andreas Motzfeldt Kravik, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alisema ushirikiano huo pia utajumuisha Mabadiliko ya Tabia Nchi, Maendeleo Endelevu na ushirikiano wa kiuchumi.

Aidha, alisemka Norway inaendelea kuunga mkono juhudi za Kenya za kutekeleza nishati safi ikiwa ni pamoja na sera ya kitaifa ya uchukuzi kutumia umeme na ushirikiano katika sekta ya uchukuzi.

“Pia tuliangazia fursa katika upanuzi wa biashara na uwekezaji, huku biashara ya panze zote mbuili ikifika dola za kimarekani Milioni 54.3 mwaka 2024,” alisema Mudavadi.

Bidhaa za Kenya ambazo huuzwa nchini Norway ni pamoja maua, kahawa, mbona na Matunda, huku Norway ikiuza nchini Kenya mbolea, bidhaa za samaki na za viwandani.

Share This Article