Kipute cha WAFCON chaahirishwa kutoka Machi hadi Julai na Agosti mwaka huu

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 16 ya kindumbwendumbwe cha mataifa ya Afrika kwa wanawake WAFCON yaliyokuwa yaanze tarehe 17 mwezi huu nchini Morocco yameahirishwa hadi kati ya Julai na Agosti.

Fainali  hizo zilizokuwa ziandaliwe kati ya tarehe 17 mwezi huu na Aprili 3 sasa zitafanyika baina ya Julai 25 na Agosti 16 mwaka huu.

Aidha, kipute hicho kitatumika kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil, huku timu zote nne zikijikatia tiketi ya Brazil mwaka ujao.

Kenya, iliyoshiriki WAFCON kwa mara ya kwanza mwaka 2016 imejumuishwa kundi A pamoja na Morocco,Algeria na Senegal katika makala ya mwaka huu.

Share This Article