Ni afueni kwa Kenya baada ya kuondolewa katika orodha ya WADA

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imepata afueni baada ya Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli Duniani (WADA), kuliondolea vikwazo Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli nchini Kenya, ADAK.

WADA kwenye taarifa imekiri kuwa Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya ulaji muku michezoni na kutimiza masharti yaliyowekwa.

Kamati ya WADA iliafikia uamuzi huo kufuatia uchunguzi wa kina wa mikakati iliyowekwa na Kenya.

Waziri wa Michezo Salim Mvurya alisifia hatua hiyo aliyosema inaashiria juhudi za serikali kumaliza utumiaji wa dawa za kusisimua misuli nchini.

Kenya kuwekwa katika orodha ya mataifa yanayochunguzwa kwa karibu na WADA ilitishia kupigwa marufuku kwa wanariadha wa humu nchini kushiriki mashindano ya kimataifa.

TAGGED:
Share This Article