Sita wafariki akiwemo Mbunge kwenye ajali ya ndege Nandi

Dismas Otuke
0 Min Read

Watu sita akiwemo Mbunge wa Emurua Dikir Johana Ng’eno wanahofiwa kufariki Jumamosi jioni katika kaunti ya Nandi kufuatia kuanguka kwa ndege ya helikopta ya kibinafsi.

Inaaminika kuwa ndege hiyo ilijaribu kutia kwa dharura kutokana na hali mbaya ya anga kabla ya kuanguka na kuteteketea.

Abiria wote sita waliokuwa wameabiri ndege hiyo wanaaminika kufa papo hapo.

Share This Article