Wanaharakati wa Kenya Bob Njagi na Nicholas Oyoo hatimaye wako huru

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanaharakati wa Kenya  Bob Njagi na Nicholas Oyooo hatimaye wako huru baada ya kuachiliwa na serikali ya Uganda Ijumaa usiku.

Kulingana na familia Njagi na Oyoo waliachiliwa huru Ijumaa usiku na kuwasilishwa katika afisi za Kamishna wa kaunti ya Busia.

Babake Longman Njagi amesema kuwa Bob aliachiliwa na kusindikizwa hadi katika mpaka wa Kenya na Uganda na baadaye kuwasilishwa kwa afisi ya
Kamishna.

Aidha, babake amekiri kuwa mwanawe yuko timamu na katika hali shwari ya kiafya.

Njagi akiwa na Mkenya mwenza  Oyoo, walitoweka nchini Uganda Septemba 30 wakiripotiwa kuwa kwenye msafara wa kampeni ya kiongozi wa
upinzani Robert Kyagulanyi, ukipenda Bobi Wine.

Ripoti ya awali iliashiria kuwa Wakenya hao wawili walishikwa mateka na wanaume waliokuwa kwenye gari katika eneo la Kamuli mashariki mwa
jiji kuu la Uganda, Kampala, na tangu wakati huo hawakujulikana waliko

Share This Article