Kamati ya bunge ya kaunti ya Kericho imependekeza kushtakiwa kwa watu sita waliohusika katika ufujaji wa shilingi milioni 14 zilizochangishwa kuwasaidia waathiriwa wa ajali ya barabarani ya Londiani.
Naibu Gavana wa kaunti ya Kericho Fred Kirui anadai shilingi milioni 13.6 zilizochangishwa kuwanufaisha wahasiriwa zimefujwa.
Yamkini watu 6 wakiwemo wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Kericho wanatuhumiwa kwa kupora pesa hizo.