Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati Ongozi ya C40, hii ikiwa taasisi inayotoa mwelekeo kwa mtandao wa dunia wa karibu miji 100 uliojitolea kuangazia janga la tabia nchi duniani.
Sakaja alichaguliwa kuwakilisha miji 13 ya C40 kutoka barani Afrika.
Tangu kuchaguliwa kwake mwaka jana, Gavana huyo ameahidi kuangazia changamoto zinazoukumba mji wa Nairobi ambao umekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na msongamano wa magari, ukosefu wa usalama na mafuriko mvua zinyeshapo.
“Kuna dharura mpya. Tunahitaji kuungana na kutafuta namna ya kufanya miji yetu kuwa imara zaidi. Na tunahitaji kufanya hili sasa hivi,” Sakaja alisema baada ya kuchaguliwa.
Katika wajibu wake mpya, Sakaja atatekeleza wajibu muhimu katika kuhamasisha miji ya Afrika kufanya kazi pamoja ili kuharakisha juhudi za kukabliana na mabadiliko ya tabia nchi.