Kenya kujadiliana upya na IMF kuimarisha uchumi wa taifa

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Kenya inajiandaa kujadiliana upya na Shirika la Fedha Duniani (IMF), baada ya muda wa mpango wa awali uliotiwa saini mwaka 2021 kukamilika.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema kuwa majadiliano hayo mapya yatalenga kuimarisha uchumi wa taifa hili kupitia  mpango wa serikali ya Kenya Kwanza wa (BETA), na kuiwianisha na miradi iliyopewa kipaumbele na serikali.

Katika mkutano na mabalozi pamoja na mashirika ya kimataifa jijini Nairobi, Mudavadi alithibitisha kuwa serikali imejitolea kuhakikisha uchaguzi mkuu unaandaliwa mwaka 2027, akidokeza kuwa mchakato wa kubuni tume mpya ya uchaguzi hapa nchini tayari umeanza.

“Kenya huandaa uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano,” alisema Mudavadi.

Katika mkutano huo, Mudavadi alielezea kujitolea kwa Kenya kuhakikisha amani, usalama, ushirikiano na utangamano wa kikanda, kama msingi wa ustawi.

Website |  + posts
Share This Article