Benki ya Sidian Kenya Limited imehamisha tawi lake la Kitui, huku ikilenga kufungua matawi 100 katika kaunti 47 mwaka huu.
Afisa Mkuu mtendaji wa wa benki ya Sidian Chege Thumbi, amesema wamehamisha tawi hilo la Kitui kutoka Mutoto Plaza Kilungya Street hadi jengo la Telyndo, ili kupeleka huduma karibu na wateja.
Benki hiyo inalenga kufungua matawi zaidi katiksa juhudi zake za kufikia kaunti zote 47 nchini.
Benki ya Sidian huwahudumia wajasiriamali wadogo kwa kuwapa nyenzo za kupanua biashara zao kupitia kwa huduma mbalimbali.