Watu 30 wafariki kwa mafuriko Kinshasa

Mji wa Kinshasa umekumbwa na mvua kubwa iliyosababisha kufurika kwa mto Ndijili unaopita katikati ya mji mkuu wa Congo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu 30 wameripotiwa kuaga dunia Jumapili mjini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha.

Mji wa Kinshasa umekumbwa na mvua kubwa iliyosababisha kufurika kwa mto Ndijili unaopita katikati ya mji mkuu wa Congo.

Yamkini, mto huo ulivunja kingo zake na kukatiza usafiri na kupotea kwa nguvu za umeme.

Taifa hilo linakumbwa na hali ya kutamausha baada pia ya zaidi ya watu 7,000, kuuawa kwenye mapigano ya wanajeshi wa serikali na kundi la waasi la M23 mjini Goma na viunga vyake.

Website |  + posts
Share This Article