Burkina Faso ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17, baada ya kujikatia tiketi kwa robo fainali ya kipute cha kombe la mataifa ya Afrika kinachoendelea nchini Morocco.
Burkinabe waliizaba Misri mabao 2-1 jana wakisajili ushindi wa pili mtaliwa kundini B.
Zambia walilazimisha sare tasa dhidi ya Morocco katika kundi A, huku Uganda ,ikiwalemea Tanzania 3-0, katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi zitakamilika leo Somalia, wakikabiliana na Gambia kundini C, kabla ya Tunisia kuhsikana mashati na mabingwa watetezi Senegal.
Katika kundi D Angola itachuana na Ivory Coast, wakati Mali wakimaliza udhia dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kundini D.
Mataifa kumi bora katika kipute hicho yatafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka huu nchini Qatar.