Moto wazuka katika soko la Gikomba

Tom Mathinji
1 Min Read
Moto wazuka kwenye soko la Gikomba.

Mali ya dhamani isiyojulikana imeteketea baada ya moto mkubwa kuzuka katika soko la Gikomba, Jijini Nairobi.

Moto huo ulizuka Jumanne alfajiri katika eneo la kuuzia mbao almaarufu ‘Kwa Mbao’ na kuharibu mali ya dhamani kubwa.

Hata hivyo chanzo cha moto huo hakijabainishwa, huku juhudi za kukabiliana na moto huo zilikuwa zikiendelea wakati wa kuchapisha taarifa hii.

Soko la Gikomba ambalo ndilo soko kubwa zaidi Jijini Nairobi lililowazi, limeghubikwa na visa kadhaa vya moto katika siku za awali, huku wafanyabiashara wakiathirika kwa kupata hasara kubwa mioto hiyo inapotokea.

Vyanzo vya moto katika soko la Gikomba, vimesalia kuwa kitendawili kisichokuwa na jawabu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article