Watu 1,700, waangamia kwenye tetemeko la ardhi Myanmar

watu 3,400 wamejeruhiwa huku wengine 300 wakiwa hawajulikani waliko kutokana na tetemeko hilo la Ijumaa iliyopita la ukubwa wa 7.7, katika vipimo vya Richa

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi ya watu waliongamia kwenye mkasa wa tetemeko la ardhi nchini Myanmar, Ijumaa iliyopita imepanda na kufikia 1,700.

Kulingana na taarifa za serikali, watu 3,400 wamejeruhiwa huku wengine 300 wakiwa hawajulikani waliko kutokana na tetemeko hilo la Ijumaa iliyopita la ukubwa wa 7.7, katika vipimo vya Richa.

Mataifa jirani ya Myanmar, yakiwemo India, China na Thailand, tayari yametuma misaada ya kibinadamu huku Malaysia, Singapore na Urusi yakituma maafisa wa uokozi.

Marekani pia imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 2 kuwasaidia wahanga.

Tetemeko hilo limeathiri miundo msingi kuu nchini humo, ikiwemo madaraja, reli, viwanja vya ndege na barabara, na kukatiza usafiri na uwasilishaji wa misaada.

Website |  + posts
Share This Article