Chadema wasimama tisti, wasema ‘hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi’

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kimekaa ngumu kikishikilia msimamo wa mabadiliko ya lazima kwa mfumo wa usimamizi wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu, amesimama kidete akisema kuwa kamwe uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hautafanyika bila  mageuzi mwafaka ya mifumo ya kusimamia na kuendesha uchaguzi.

Lissu amesema mfumo wa sasa una mapendeleo kwa Rais Samia Suluhu wa Chama cha Mapinduzi – CCM na kutaka mabadiliko ya haraka kabla ya uchaguzi mkuu.

Katika mkutano wa kisiasa mkoani Songwe jana Alhamisi, Lissu alielezea bayana azma yake na chama chake kuzuia uchaguzi endapo hapatakuwepo na uhuru na uwazi wa mfumo wa usimamizi wa zoezi hilo.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania, inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, ambapo Rais Samia atatetea kiti chake kwa tiketi ya CCM.

Website |  + posts
Share This Article