Taasisi zinazofunza maswala ya lishe zatakiwa kuwa na maabara maalum

Tom Mathinji
1 Min Read

Taasisi zote za mafunzo za umma na za kibinafsi zilizo na leseni ya kutoa kozi za lishe, zimepewa miezi sita kupata maabara za ujuzi maalum zilizoidhinishwa.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wataalamu wa Lishe, Dkt David Okeyo, alisema  kuwa maabara za ujuzi zilikosekana katika taasisi nyingi za mafunzo hivyo kuathiri mahitaji ya mafunzo kwa wanafunzi.

Dk. Okeyo alisema  kuwa maabara zilizoidhinishwa zilikuwa na ufundi wa hali ya juu unaohitajika kwa ujuzi wa awali wa mafunzo ya wataalamu wa lishe.

Akizungumza akiwa eneo la Mlolongo kaunti ya Machakos, Dkt. Okeyo alifichua kuwa ni vyuo vinne pekee vya mafunzo vilivyoidhinishwa kati ya 83 vilivyopata vifaa hivyo vya mafunzo, hali ambayo alisema inatia wasiwasi.

Profesa Gordon Nguka ambaye ni mjumbe wa baraza la KNDI anayesimamia uidhinishaji alitoa changamoto kwa taasisi za mafunzo kupata vifaa vinavyohitajika vya maabara.

Alisema vifaa hivyo ni muhimu katika kuimarisha mafunzo yanayozingatia umahiri katika fani ya lishe.

Chuo Kikuu cha Mt. Kenya, Chuo cha Nuria, Taasisi ya Kitaifa ya Ufundi ya Kabete na Taasisi ya mafunzo ya Visions Empowerment  ndizo taasisi za pekee za mafunzo ambazo zimepata maabara zilizo na vifaa kamili.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *