KUPPET yatishia kugoma ikiwa pesa hazitatolewa kwa shule

KUPPET inatishia kuwashauri walimu wakuu kufunga shule ikiwa fedha hazitatolewa na serikali haraka iwezekanavyo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo, KUPPET, kimetishia kuitisha mgomo wa kitaifa endapo serikali haitatoa fedha za kufadhili elimu kwa shule za sekondari ndani ya wiki moja ijayo.

Kwenye kikao na wanahabari, KUPPET imeelezea masikitiko yake kuwa shule hazijapata pesa za muhula wa kwanza, wiki mbili tangu zifunguliwe.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Moses Nthurima amesema kuwa shule nyingi  zimeshindwa kulipa watoa huduma.

“Tunataka serikali itoe pesa shuleni ndani ya siku saba sijazo la sivyo tutawashauri walimu wakuu wafunge shule,”alitishia Nthurima.

Hali ni vivyo hivyo katika vyuo vikuu vya umma ambapo wanafunzi wamekuwa wakiilaumu serikali kwa kuchelewa kutoa fedha za kuwawezesha kuendelea na masomo yao.

Wanafunzi hao wameelezea hofu kuwa hatua hiyo itasababisha wao wazuiwe na vyuo vyao husika kufanya mitihani.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *