Mawaziri watatu wapya wataapishwa leo Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa jana.
Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, ambaye alihudumu kama Waziri wa Afya katika serikali iliyopita, William Kabogo aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali pamoja na Waziri wa Biashara Lee Kinyanjui, watakula viapo vya utendakazi kuanzia majira ya saa nne asubuhi.
Watatu hao waliidhinishwa na kamati ya bunge kabla ya bunge lote kuwaidhinisha jana.
Kagwe anarithi Wizara ya Kilimo kutoka kwa mtangulizi wake Dkt .Andrew Karanja, Kabogo akitwaa mikoba kutoka kwa Dkt. Maragaret Ndung’u huku Kinyanjui akishika hatamu za kuoingoza Wizara ya Biashara kutoka kwa Salim Mvurya aliyehamishiwa katika Wizara ya Michezo.