Wabunge watarejelea vikao leo baada ya kusitisha likizo ya muda mrefu ili kutathmini ripoti ya kamati ya bunge iliyowapiga msasa Mawaziri watatu wapya.
Mawaziri watatu walioteuliwa na Rais William Ruto katika serikali jumuishi ni William Kabogo, Mutahi Kagwe na Lee Kinyajui.
Wote hao watabaini hatima yao leo baada kikao hicho cha bunge.
Endapo Mawaziri wateule Kagwe katika Wizara ya Kilimo, Kabogo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi Dijitali na Kinyanjui wa Biashara wataidhinishwa na bunge, watakuwa huru kula kiapo cha majukumu yao.
Kamati ya bunge la kitaifa pia itawasilisha ripoti ya Mabalozi wateule na uteuzi wa Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Wabunge wamekuwa katika likizo ndefu ya miezi miwili kabla ya kuitwa na Spika Moses Wetang’ula.
.