Portable aonya wanaomfananisha na Asake, asema anafanana Lil Wayne

Alisema hayo kwenye video aliyochapisha kwenye Instagram.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Nigeria Habeeb Olalomi Badmus maarufu kama Portable, ameonya mashabiki wake ambao wanamfananisha na mwanamuziki mwenza Asake, huku akiwataka wakome.

Portable alichapisha video kwenye Instagram ambapo anasikika akisema yeye anafanana na mwanamuziki wa Marekani Lil Wayne na kwamba ni yeye pekee nchini Nigeria na Barani Afrika anamfanana.

Alijigamba pia kwamba yeye sasa ni mwanamuziki wa kimataifa na kwamba utajiri wake hautokani na kampuni ya Empire records, ambayo inasimamia Asake.

Yeye anasema pesa anazofurahia zinatoka kwa kampuni ya Sony. Alijirejelea kama mkurugenzi mtendaji na kwamba Sony haiwezi kumharibia sifa sawa na Empire records kwani hakuchukua pesa zao.

Katika video hiyo, Portable alitaja na kushukuru wasanii ambao walimsaidia na kuhakikisha anakua katika tasnia ya muziki akisema mpaka sasa anafaidi kifedha kutokana na usaidizi huo.

Wasanii hao ni pamoja na Olamide, Skepta na Wizkid.

Alielezea kwamba bado anapokea pesa kutokana na kibao ‘Zazuu’ ambacho alimshirikisha Olamide. Alikutana na Skeptahuko London na anasema alibadili maisha yake.

Portable alifafanua kwamba Skepta alimwonyesha njia na kwa sababu yake anapokea malipo kutoka kwa kampuni ya Sony Records.

Kuhusu Wizkid, Portable alisema aliwahi kumpa pesa na alifanya asakwe kama mwanamuziki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *