Rais William Ruto amekutana na Gavana wa zamani wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi katika Ikulu ya Nairobi.
Mkutano kati yao unakuja siku chache baada ya Murungi kukutana na Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kipchumba Murkomen.
Mkutano kati ya Rais Ruto na Murungi huenda ukachambuliwa kuwa njama ya kiongozi wa nchi kutafuta uungwaji mkono wa eneo la Mlima Kenya.
Unngwaji mkono wa serikali ya Kenya Kwanza katika eneo hilo umesemekana kuyumbayumba tangu kutimuliwa madarakani kwa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachaga.
Kiraitu ameonekana kuyumbayumba kisiasa katika siku za hivi karibuni, nyakati zingine akionekana kuikosoa serikali ya Kenya kwanza kwa kuzembea kazini.