Mwigizaji wa Nigeria Regina Daniels alimrejelea mamake kama ‘mungu wake wa humu duniani’ alipokuwa akimtakia mema kwenye kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Regina alichapisha picha kadhaa za pamoja na mamake na kuandika, “Siku njema ya kuzaliwa mfalme wangu wa kike. Mlezi na mlinzi wangu duniani. Rafiki yangu mmoja wa kweli, mshauri, mama na rafiki wa kufa kupona.”
Aliendelea kumsifia mamake mzazi akisema milele ataendelea kubariki uwepo wake duniani huku akiabudu anakokanyaga.
“Wewe ni kila kitu na zaidi katika mama na ninashukuru Mungu kwa zawadi yako. Nitachagua kuwa binti yako kila mara, ili uendelee kunielekeza vyema.” aliendelea kusema mama huyo wa watoto wawili.
Regina ambaye alianza kuigiza akiwa mtoto mdogo alisimulia jinsi yeye na mamake walipitia mengi na wanaendelea kupitia mengi pamoja huku akiomba Mungu ampe nguvu, afya nzurina masiha marefu.
Binti huyo ana uhusiano wa karibu sana na mamake na uvumi ulisambaa kwamba yeye ndiye alikutanisha Regina na mume wake mkwasi Ned Nwoko ambaye pia ni Seneta.
Wawili hao huandamana kila mahali hadi kwenye chumba cha kujifungua, kulingana na picha alizochapisha Regina.