Rais Ruto asisitiza ushirikiano wa Afrika katika kuwa na mifumo thabiti ya chakula

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo kwenye kongamano la Umoja wa Afrika kuhusu maendeleo ya kilimo jijini Kampala nchini Uganda.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto amesisiriza haja ya mataifa ya Afrika kushirikiana kuunda mifumo thabiti ya chakula kama sehemu ya juhudi zinazoendelea za kumaliza njaa katika bara hili.

Rais Ruto alikiri kwamba watu wengi Barani Afrika hawajahakikishiwa usalama wa chakula na hivyo kuna haja ya nchi kuwekeza katika miundombinu, uvumbuzi na Teknolojia ili kukabiliana na changamoto.

Lengo la hatua hiyo kulingana naye ni kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha lishe bora, kuimarisha mifumo endelevu itakayolinda mustakabali wa dunia na kufanya kilimo kuwa chanzo cha ajira na ufanisi.

Rais alisema hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuboresha maisha, kulinda mazingira na kutimiza jukumu muhimu la kulisha Bara Afrika.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo kwenye kongamano la Umoja wa Afrika kuhusu maendeleo ya kilimo jijini Kampala nchini Uganda.

Kando kando mwa kongamano hilo, Rais Ruto alifanya mkutano na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambapo viongozi wote wawili walikubaliana kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuimarika.

Rais Ruto alifafanua kwamba kufuatia uhusiano huo bora, nchi hizo zinafanya biashara kati yazo kuliko ilivyokuwa awali ambao Somalia ilinunua bidhaa za thamani ya shilingi bilioni 5 miwezi 9 ya kwanza ya mwaka 2024.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *