Watatu wafariki huku 41 wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani Londiani

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu watatu wamefariki mapema leo huku wengine 41 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea kwenye barabara ya Londiani-Kisumu.

Kulingana na taarifa ya polisi, ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi alfajiri baada ya dereva wa basi la Dreamliner kupoteza mwelekeo na kuanguka kwenye mtaro.

Abiria 41 waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Londiani wanakopokea matibabu.

Walioaga dunia ni pamoja na watu wazima wawili na mtoto mmoja.

Polisi wamesema dereva wa basi la Dremaliner alijaribu kukata kona aliposhindwa kulidhibiti na likatumbukia kwenye mtaro.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *