Shule nyingi zabainika kutokuwa na uwezo wa kumudu Gredi ya 9

Marion Bosire
1 Min Read

Shule nyingi za umma na binafsi hazitakuwa na uwezo wa kutekeleza masomo ya Gredi ya 9 kwa ufanisi kutokana na ukosefu wa miundombinu na walimu waliohitimu.

Akizungumza katika shule ya Earlybird Junior School huko Machakos, mkuu wa shule James Kamuya alieleza kuwa shule nyingi hazina uwezo wa kujenga madarasa yanayohitajika katika shule zote za umma na binafsi.

Hata hivyo, hali ni tofauti kwao kwani wameweza kujenga madarasa mapya manne na kutoa vifaa vya kutosha kwa wanafunzi wao.

Kamuya sasa anaiomba serikali ya kitaifa kupitia kwa wizara ya elimu kupeleka fedha zaidi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kuwapa walimu vifaa ili kutekeleza mfumo wa gredi ya 9 nchini.

Alielezea kwamba shule nyingi hazina nafasi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Kuhusu mfumo wa elimu wa CBC, mwalimu huyo alisema ni bora kwa kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi, na serikali inapaswa kuunga mkono kikamilifu mfumo huu katika shule zote za umma na binafsi.

Shule ya Earlybird huko Machakos ni moja kati ya shule chache ambazo zimekidhi mahitaji ya gredi ya 9 na ina madarasa manne yanayotumika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *