CAF yaongeza zawadi ya pesa kwa washindi wa CHAN mwaka huu kwa asilimia 75

Dismas Otuke
1 Min Read

Zawadi ya pesa kwa washindi wa makala ya mwaka huu ya fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) imeongezwa kwa asilimia 75 .

Hii ina maana kuwa washindi wa kipute hicho kitakachoandaliwa kwa pamoja na Kenya,Uganda na Tanzania watatia kibindoni dola milioni 3.5 za Marekani, sawia na shilingi milioni 452.3 za Kenya.

CAF pia imeongeza zawadi ya pesa zitakazoshindaniwa kwa asilimia 32 hadi dola milioni 10.4, sawa na shilingi bilioni 1.344 za Kenya.

Fainali za CHAN zitaandaliwa Afrika mashariki kuanzia Februa 1 hadi 28 mwaka huu.

Mataifa 17 yamefuzu yakiwemo waandalizi watatu :Kenya,Uganda na Tanzania pamoja na Morocco, Guinea, Senegal, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Nigeria, Central African Republic, Democratic Republic of Congo, Congo, Sudan, Zambia, Angola na Madagascar.

Timu mbili za mwisho kufuzu zitabainika baada ya mechi mbili za mwisho zitakazochezwa.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *