Karua aruhusiwa kumwakilisha Besigye

Dismas Otuke
1 Min Read

Baraza la Wanasheria nchini Uganda limebatilisha uamuzi wake wa awali na kumruhusu Martha Karua, kuwa mmoja wa mawakili wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt. Kizza Besigye na msaidizi wake Hajj Obeid Lutale katika mahakama ya kijeshi.

Dkt. Bisigye na Lutale wanatarajiwa kurejea katika mahakama ya kijeshi jijini Kampala leo Jumanne.

Hii ni baada ya kuwekwa rumande kwa majuma kadhaa baada ya kutekwa nyara mwezi Novemba mwaka jana na watu wasiojulikana wakiwa nchini Kenya.

Baraza hilo awali lilikataa kumuidhinisha Karua kuwa wakili kwenye kesi hiyo, kwa kusema kuwa ombi lake halikufuata utaratibu ufaao na pia lilichochewa kisiasa.

Dkt. Bisigye na Lutale wanakabiliwa na kesi ya kuhataraisha usalama wa kitaifa na pia kumiliki  silaha bila leseni.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *