Wakenya kunufaika na huduma za kupandikiza figo katika hospitali ya KUTRRH

Tom Mathinji
1 Min Read
Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Chuo Kikuu cha Mafunzo na Rufaa cha Kenyatta (KUTRRH), kina mipango ya kuanzisha upasuaji wa kupandikiza figo katika muda wa mwezi mmoja ujao, kuashiria hatua kubwa iliyopigwa kama taasisi ya kwanza ya matibabu hapa nchini kuwa na huduma aina hiyo.

Hatua hii inalenga kuwapunguzia mzigo wakenya ambao hutafuta huduma za upandikizaji wa figo katika mataifa ya ng’ambo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa hopsitali hiyo Dkt.. Zainab Gura, alitangaza kuwa mipango yote ya kuanzisha huduma hiyo ya kihistoria imekamilika, ili kuwafaidi wagonjwa walio na matatizo ya figo.

Dkt. Gura aliyasema hayo wakati wa siku ya kuadhimisha ugonjwa wa figo duniani, yaliyoandaliwa katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa huduma za afya Dkt. Patrick Amoth, alisema Halmashauri ya Afya ya Jamii SHA, sasa itagharamia matibabu ya upandikizaji wa figo kikamilifu.

SHA pia itagharamia huduma za kabla na maada ya matibabu.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *