Ruto kuhudhuria uapisho wa Rais Mahama wa Ghana leo

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto alipotembelewa na Rais mteule wa Ghana John Mahama mwaka jana

Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama leo Jumanne jijini Accra, Ghana.

Ruto aliondoka nchini jana Jumatatu tayari kwa shughuli ya leo.

Rais mteule Mahama alimwalika Ruto kwa uapisho wake alipomtembelea nyumbani kwake Narok tarehe 29 mwezi uliopita.

Mahama aliye na umri wa miaka 66 alihudumu kwa muhula wa kwanza  baina ya mwaka 2012 hadi 2017, akitwaa uongozi kufuatia kifo cha  Rais John Atta Mills, kabla ya kushindwa na Nana Akuffo Addo mwaka 2017.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Mahama alipata asilimia 98 ya kura dhidi ya mpinzani wake Kojo Bonsu, aliyepata chini ya asilimia 2.

Ruto na mwenyeji wake Mahama wanatarajiwa kujadiliana maswala kadhaa ikiwemo ushirikiano katika sekta za nishati, nguo, diplomasia na biashara.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *