Kipyegon ateuliwa kuwania tuzo ya Laureus kwa mwaka wa pili mtawalia

Aidha Kipyegon alishinda medali ya fedha ya Olimpiki katika mita 5,000.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon, ameteuliwa kuwania tuzo ya Laureus ya mwanaspoti bora kwa wanawake mwaka huu.

Ni mwaka wa pili mtawalia kwa bingwa huyo mara tatu wa dunia katika mbio za mita 1,500, kujumuishwa kwenye orodha ya waaniaji wa tuzo ya Laureus.

Kipyegon aliye na umri wa miaka 31, alikuwa na msimu wa kufana mwaka jana akishinda dhahabu ya Olimpiki katika mita 1,500 jijini Paris Ufaransa, akiweka rekodi ya Olimpiki, ikiwa taji ya tatu mtawalia katika shindano hilo.

Aidha Kipyegon alishinda medali ya fedha ya Olimpiki katika mita 5,000.

Hafla ya mwaka huu itaandaliwa mjini Madrid, Uhispania, Aprili 21 mwaka huu, ikiambatana na maadhimisho ya miaka 25 tangu kuasisiwa kwa tuzo hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *