Aliyekuwa mshambulizi wa zamani wa Afrika Kusini Benedict Saul McCarthy, almaarufu Benni McCarthy, anatarajiwa kuzinduliwa leo Jumatatu kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya, Harambee Stars.
McCathy, ambaye ni mfungaji bora wa Bafanabafana kwa magoli 31, atatwaa ukufunzi wa Kenya kutoka kwa kaimu kocha Francis Kimanzi.
McCarthy, aliye na umri wa miaka 47, anatarajiwa kuandamana na wasaidizi wake akiwemo mkufunzi wa makipa huku pia akitarajiwa kuhudhuria debi ya mashameji kati ya AFC Leopards na Gor Mahia Jumapili hii kuwania alama 3 za Ligi Kuu.
Yamkini McCarthy ataandamana na kipa wa zamani wa timu ya Afrika Kusini na pia kilabu ya Orlando Pirates Moneeb Josephs na Vasili Manousakis watakaokuwa wakufunzi wa walinda lango.
Wasifu wa McCarthy
Alizaliwa: Novemba 12 mwaka 77 (Umri miaka 47) mjini Cape Town
Aliichezea klabu ya Seven Stars mwaka 1996, kabla ya kujiunga na Capetown kwa mkopo
1998 – Alirejea Sevens Stars mwaka 1998
1997/1998 – Alihama Seven Stars na kujiunga na Ajax Amsterderm ya Uholanzi
1999/2000 – Aligura Ajax na kujiunga na Celta Vigo ya Uhispania
2002 – Alihama Celta Vigo na kujiunga na FC Porto ya Ureno kwa mkopo
2003 – Alirejea Celta Vigo baada ya kumalizika kwa mkopo wa Porto
2023 – Ajiunga na FC Porto
2006 – Alihamia Blackburn Rovers ya Uingereza kutoka FC Porto
2010 – Ahima Rovers na kujiunga na Westham United ya Uingereza
2011 – Alisalia bila klabu baada ya kutemwa na Westham United
2015 – 2016 – Alikuwa naibu meneja wa klabu ya Sint Truiden ya Ubelgiji
2017-2010 – Meneja wa klabu ya Cape Town City
2021-2022 – Menaja klabu ya AmaZulu FC
2022-2023 – Kocha wa Washambulizi Manchester United FC
Kibarua cha kwanza kwa kocha huyo mpya ni kuingoza Harambee Stars kwa mechi ya kundi F, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao dhidi ya Gabon mechi ya mwezi huu jijini Nairobi.
Kenya ni ya nne kundini kwa alama 5, nyuma ya Ivory Coast, Gabon, na Burundi zilizo na alama 10, 9, na 7 mtawalia.