Makanisa manane yameungana kukabiliana na umaskini na kuinua hali ya wakazi wa mji wa Nyahururu kiuchumi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana mjini humo.
Mpango huo unaendeshwa chini ya mwavuli unaoitwa Mchakato wa Pamoja wa Kanisa na Jamii (CCMP).
Makanisa hayo yanalenga kutumia rasilimali zinazopatikana eneo hilo kuangamiza umaskini na kuinua viwango vya maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Makanisa yanayoshiriki mpango huo ni pamoja na Anglican Church of Kenya (ACK), African Brotherhood Church (ABC), African Christian Church and Schools (ACC&S), African Inland Church (AIC) na African Interior Church (AIC).
Mengine ni Friends Church, Pentecostal Evangelical Fellowship of Africa (PEFA) na Redeemed Gospel.
Shangwe na vigelegele viliitawala anga wakati mpango huo ulipozinduliwa na Dayosisi ya kanisa la ACK mjini Nyahururu katika hafla iliyoongozwa na Askofu Samson Gachathi mjini Nyahururu.
Taarifa ya Lydia Mwangi