Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi Dijitali, William Kabogo, leo amefika mbele ya kamati ya bunge ya Habari, Mawasiliano na Uvumbuzi kuhusu kujumuishwa kwa sera za wizara hiyo katika bajeti ya serikali.
Waziri Kabogo aliandamana na makatibu katika wizara hiyo; John Tanui wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na mwenzake wa utangazaji na mawasiliano ya simu Prof. Edward Kisiangani, na wawakilishi kutoka kwa idara mbalimbali za wizara hiyo.
Kabogo alielezea kamati hiyo ya bunge kuhusu ufanisi na changamoto wizara yake inakumbana nazo katika utekelezaji wa bajeti.
Kamati hiyo ya bunge inayoongozwa na mbunge wa Dagorethi Kusini John Kiarie, iliahidi kumuunga mkono Waziri hiyo katiaka kuharakisha utekelezaji wa mipango yake ili kupiga jeki maendeleo ya kiuchumi.