Washindi mara 12 wa taji ya ligi ya mabingwa Afrika, klabu ya Al Ahly SC itamenyana na Al Hilal ya Sudan katika robo fainali ya kombe hilo.
Kulingana na droo iliyoandaliwa jana mjini Doha, Qatar Pyramids ya Misri itapambana na AS FAR kutoka Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikabane koo na Esperance ya Tunisia, huku MC Alger ya Algeria, ikipimana nguvu na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Mshindi wa robo fainali kati ya Ahly na Hilal atachuana na mshindi baina ya Esperance na Mamelodi katika nusu fainali ya kwanza.
Nusu fainali ya pili itawakutanisha mshindi kati ya Alger na Pirates na atalayeshinda baina ya Pyramids na AS FAR.
Mkondo wa kwanza utaandiliwa tarehe 1 Aprili huku marudio ikiwa wiki moja baadaye.