Ugali wasababisha mauti eneo la Likuyani, Kakamega

Carolyn Necheza
1 Min Read

Hali ya majonzi imegubika kijiji cha Kilimani, kata ndogo ya Seregeya katika eneo bunge la Likuyani, kaunti ya Kakamega baada ya mwanamume mmoja kudaiwa kumuua nduguye kwa kumkatakata kwa shoka. 

Hii ni baada ya wawili hao kudaiwa kuzozania ugali.

Kwa mujibu wa Peter Lukala, nduguze Michael Lukala na Reuben Lutabony walishinda pamoja wakichimba kisima katika kijiji jirani.

Hata hivyo, tofauti iliibuka baina yao walipokuwa wakipika ugali kabla ya Reuben kumshambulia Michael na kumkatakata mara kadhaa kichwani.

Ni shambulizi lilosababisha kifo cha Michael papo hapo.

Kwa upande wake, mama yao Esther Akwam anasema alijaribu kuwatenganisha wanawe ila alizidiwa baada ya kusukumwa na kufungiwa nje ya nyumba.

Mzee wa mtaa wa eneo hilo Cleophas Barasa ameelezea kusikitishwa na kisa hiki akiwataka ndugu kutafuta njia mwafaka ya kusuluhisa tofauti baina yao badala ya maafa kama hayo.

Carolyn Necheza
TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *