Wafanyakazi zaidi ya 57 wa hospitali ya kaunti ndogo ya Kimilili katika kaunti ya Bungoma waligoma leo Jumatatu kulalamikia kutolipwa mishahara yao kwa muda wa miezi sita.
Wakiwahutubia wanahabari, wafanyakazi hao waliopandwa na mori wamemtaka Gavana Ken Lusaka kuwalipa mishahara hiyo ili wamudu hali ya maisha wanayosema imekuwa ni ngumu zaidi.
”Mimi naitwa Jackline Wekesa Wanyama. Nafanya kazi hapa na nina uchungu sana kwa kukosa mishahara, tunaishi nyumba za kulipa, watoto wetu hawaendi shule kwa kukosa karo, tunaomba Mheshimiwa Ken Lusaka popote ulipo, sisi ni kama dada zako. Utukumbuke kwa sababu tunaumia, mishahara tunalipwa mara mbili kwa mwaka. Je, ni nani hulipwa hivyo? ” alilalamika Wanyama.
Taarifa yake Boniface Musotsi