Rais wa Angola João Lourenço ndiye mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika,AU akimrithi Mohamed Cheikh El Ghazouani wa Mauritania ambaye amekuwa usukani tangu Februari mwaka jana.
Lourenço atahudumu kwa mwaka mmoja akisaidiwa na manaibu wake kutoka mataifa ya Burundi, Ghana na Tanzania kama manaibu wa kwanza pili na tatu mtawalia.
Uenyekiti wa AU hupokezwa kwa zamu kwa maeneo yote matano ya Afrika.