Serikali inatumia mikakati mitatu kubuni nafasi za ajira nchini, asema Kindiki

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali ya Kenya Kwanza inatumia mikakati mitatu kubuni nafasi za ajira humu nchini. 

Kenya inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira, hali ambayo imelaumiwa kwa kuchangia visa vya uhalifu huku Wakenya wengi wakiazimia kutafuta ajira ughaibuni.

“Serikali inatoa kipaumbele katika kubuni nafasi za ajira kwa watu wa Kenya kupitia mikakati mitatu inayojumuisha mipango ya nyumba za gharama nafuu na mipango mingine, ajira za dijitali kupitia kuanzishwa kwa vituo vya ICT na kutafuta kampuni za kibiashara na mpango wa kutafuta ajira ughaibuni,” amesema Kindiki.

Ameyasema hayo katika makazi ya Naibu Rais mtaani Karen leo Alhamisi wakati wa mkutano wa kwanza wa kupatiwa taarifa za kiufundi kutoka kwa taasisi kinara zinazoshughulika na masuala ya ajira.

Kongamano la serikali nzima la mashauriano juu ya ufuatiliaji na uwajibikaji wa masuala ya kubuni ajira limepangwa kufanyika wiki ijayo.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *