Watatu wafariki katika ajali ya lori Murang’a

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu watatu waliaga dunia kwenye ajali ya lori mapema jana Jumanne kwenye barabara ya Karaianii-Kangema eno la Mathioya, kaunti ya Murang’a.

Polisi wamethibitisha ajali hiyo wakisema kuwa dereva wa lori hilo alipoteza mwelekeo baada ya breki kukataa kufanya kazi na kutumbukia ndani ya mtaro.

Lori hilo pia liliwajeruhi watoto kadhaa waliokuwa kando ya barabara huku 16 wakipokea matibabu hospitalini na hawapo hatarini.

Mmoja wa vijana waliojeruhiwa alifariki akipokea matibabu hospitalini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *