Serikali imetangaza kubuniwa kwa kaunti ndogo 27, divisheni 59, kata 170 na kata ndogo 322 kote nchini.
Akitoa tangazo hilo, Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amesema lengo la kubuni maeneo hayo mapya ya utawala ni kurahisisha udumishaji usalama na kuleta huduma za serikali karibu na wananchi.
Kaunti ndogo 27 zilizobuniwa ni pamoja Magarini South, Magarini North, Kokane, Assa, Akachiu, Maua, Tharaka West, Kibung’a, Mukothima, Ndithini,Kiatineni Market, Nuu na Zombe.
Nyingine ni pamoja na Illeret, Engineer, Soin,Kipsitet, Sigowet, Chepkemel, Kolowa huku makao makuu yakiwa ni – Kolowa, Baringo West, Barwesa, Mukutani, Mukutani, Tiaty Central, Chemolingot na Samburu West.
Kaunti nyingine ndogo ni North East Kano, Masogo, Ndhiwa East, Ndhiwa West, Siaya West, Uranga, Embakasi East, Embakasi West na Embakasi North.
Nyingine ni Embakasi South, Roysambu na Ruaraka.
Mabadiliko hayo yameathiri kaunti 31 kote nchini na ni mabadiliko yaliyokuwa yametangazwa na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki mwezi Februari mwaka huu.