Watu wanne wakamatwa na pembe za ndovu Busia

Marion Bosire
1 Min Read

Washukiwa wanne wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Busia baada ya kupatikana na vipande 10 vya pembe za ndovu.

Vipande hivyo vina uzani wa kilo 28 na thamani yake inakisiwa kuwa shilingi milioni 2.8.

Afisa mkuu wa upelelezi wa jinai katika kaunti ya Busia Benson Omondi alielezea kwamba walipata habari kutoka kwa wananchi na wakafanikiwa kukamata washukiwa ambao walikuwa wanatafuta mnunuzi.

Maafisa wa usalama wakiwemo maafisa wa kitengo cha kutunza wanyama pori walitekeleza msako katika eneo la Mundika walikomatwa washukiwa.

Wanne hao wanasubiri kufikishwa mahakamani huku wakazi wakionywa dhidi ya biashara haramu na kishauriwa kujihusisha na biashara halali.

Ni hatia kuuza na kununua vipande vya sehemu za miili ya wanyama pori nchini Kenya kwa lengo la kulinda wanyama hao wasiangamizwe kabisa kupitia uwindaji haramu.

Website |  + posts
Share This Article