Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula jana jioni alimuaga rasmi Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian, ambaye amekamilisha kipindi chake cha kuhudumu cha miaka minne.
Wetang’ula alisifia juhudi za Balozi Zhou za kuimarisha ushirikiano baina ya Kenya na China kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo mawili.
“Leo nimemuaga rafiki yangu wa muda mrefu na mtumishi mkubwa aliyejitolea kuimarisha ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya nchini zetu mbili”,akasema Wetangula
“Balozi Zhou amekuwa muhimili mkuu kuhakikisha Kenya na China zinashirikiana katika sekta za maendeleo kama vile uchumi,elimu,teknolojia ya usalama na sekta nyinginezo pamoja na ushirikiano wa viwango vingine vikuu”. akasema Spika Wetang’ula
Upande wake Balozi huyo alipongeza ushirikiano ambao umekuwepo kati ya China na Kenya katika kipindi chake cha kuhudumu.
“Nashukuru sana fursa niliyoipata kuhudumu nchini Keny,a hatua za ushirikiano tulizoziafikia kwa pamoja .Nilikuwa Balozi wa kwanza kuzuru ofisi yako baada ya kuchaguliwa kwako na nimefurahia ushirikiano wangu mzuri na wewe Bwana Spika,nashukuru kwa hilo”,akasema Balozi Zhou
Balozi huyo pia amepongeza juhudi za bunge la Kenya akihimiza ushirikiano zaidi kati ya bunge la Kenya na lile la China ili kubadilishana mawazo na maarifa.