Uamuzi wa pamoja wampa Jake Paul ushindi dhidi ya Mike Tyson

Tom Mathinji
1 Min Read
Jake Paul amshinda Mike Tyson katika pambano la uzani wa juu.

Jake Paul alimshinda bingwa wa ndondi za uzito wa juu Mike Tyson katika pambano lililosubiriwa kwa hamu, lililoandaliwa kupitia Netflix.

Paul alipata ushindi huo kupitia uamuzi wa pamoja wa majaji baada ya wanamasumbwi hao kupambana kwa raundi nane, mbele ya mashibi takriban 70,000 huku mamilioni wakitazama kupitia Netflix.

Baada ya kutangazwa mshindi, Paul alimsifu Tyson akisema,”Nimetiwa moyo na Tyson, bila yeye hatungekuwa hapa leo.”

Kwa upande wake, Tyson alimtaja Jake Paul kuwa mpiganaji mzuri, huku akimpongeza kutokana na ujuzi wake wa kupigiwa mfano.

Mike Tyson alipigana mara ya mwisho 2005, ambapo ameshindwa mara saba kwenye rekodi yake ya kitaaluma.

Kwa Jake Paul huu ni ushindi wa 11 Kati ya mashindano 12 aliyowahi kufanya.

Website |  + posts
Share This Article