Serikali haitaingilia uchaguzi ujao wa Shirikisho la Soka humu nchini unaotarajiwa kuandaliwa Disembe 7,2024, lakini washikadau wote wanaohusika lazima wazingatie sheria.
Katibu katika wizara ya Michezo Peter Tum alisema kwamba wagombezi ambao wamezuiwa na sheria kutafuta muhula mwingine wa uongozi hawataruhusiwa kugombea viti.
Tum alisema hayo alipoungana na familia na marafiki wa aliyekuwa mchezaji wa Gor mahia na gwiji wa kimataifa Austin Oduor kwenye hafla ya mazishi yaliyofanywa leo katika kijiji cha Makunga, Kaunti ya Kakamega.
Oduor, beki mashuhuri aliyeongoza Gor mahia kunyakua taji ya Afrika, alisifiwa kama kiongozi wa kupigiwa mfano ambaye vitendo vyake vinapigiwa mfano ndani na nje ya uwanja.
Marehemu Austin Oduor ameacha Mjane, watoto sita akiwemo kipa wa awali wa harambee stars Arnold Origi na wajukuu kadhaa.