Sera ya kigeni ya Kenya: Mudavadi atafuta ushauri wa kamati ya bunge

Martin Mwanje
1 Min Read

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi amefanya mashauriano na Kamati ya Bunge la Taifa juu ya Ulinzi, Ujasusi na Uhusiano wa Kigeni. 

Kiini cha mashauriano hayo kilikuwa ni mchakato unaoendelea wa kuipitia upya sera ya kigeni ya nchi hii.

Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje amesema wizara hiyo inaendeleza juhudi za waraka uliopitiwa upya wa sera hiyo kufanywa kuwa taarifa ya sera itakayowasilishwa bungeni.

Dhamira ya hatua hiyo ni kuhakikisha nchi hii ina mpangokazi madhubuti wa sera ya kigeni unaoeleweka na unaofaa.

Wakati wa kikao na wanachama wa kamati hiyo, Mudavadi alisema bunge hutekeleza wajibu muhimu katika kuunda na kusimamia sera ya kigeni ya nchi hii kwa kuhakikisha inawiana na maslahi ya taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje kwa sasa inaandaa makongamano ya kutafuta ushauri juu ya juhudi zinazoendelea za kuipitia upya sera hiyo.

Website |  + posts
Share This Article