Pande husika Sudan Kusini zakubali kurejelea mazungumzo ya upatanishi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akiwa Juba, Sudan Kusini.

Pande husika kwenye mchakato wa amani nchini Sudan kusini zimekubaliana kurejelea mashauriano ya upatanishi jijini Nairobi ili kushughulikia maswala yaliyosalia.

Mkataba huo uliafikiwa wakati wa mkutano wa maafisa wa ngazi za juu kuhusu mpango wa kuleta amani wa Tumaini jijini Juba, Sudan kusini, baina ya rais Ruto na rais Salva Kiir Mayardit.

Makamu wa kwanza wa rais nchini Sudan kusini, Riek Machar, alihudhuria mashauriano hayo.

Viongozi hao wawili walielezea kuridhika kwao kwamba pande zianzozozana zimeafikia makubaliano kuhusu maswala tisa.

Ili kuhitimisha mchakato wa upatanishi viongozi hao wawili waliagiza kwamba kundi la upatanishi likutane tena na kusuluhisha maswala yaliyosalia katika muda wa majuma mawili.

Rais Ruto alisema ni jambo la kutia moyo kwamba mapengo baina ya serikali na upinzani yanaweza kuzibwa na hivyo kufanikisha enzi mpya ya amani na ustawi endelevu.

Kadhalika walikubaliana kuhusisha shirika la (IGAD) kwneye mchakato huo na kuungwa mkono na jamii ya kimataifa katika kanda hiyo na duniani.

Marais hao wawilli walisema kuwa barabara ya umbali wa kilomita 11 kutoka Nadapal hadi Nakodok ni muundo msingi muhimu baina ya nchi hizi mbili katika kuimarisha biashara na usafiri baina ya nchi hizi mbili.

Share This Article