Mvurya: Kenya inabuni mifumo thabiti ya utoshelevu wa chakula

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa biashara na uwekezaji Salim Mvurya.

Waziri wa uwekezaji, biashara na viwanda Salim Mvurya, leo Jumatano aliongoza ujumbe wa ngazi za juu katika kongamano la ‘Ulimwengu Bila Njaa 2024’, Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu ustawi wa viwanda (UNIDO), Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), na shirika la kilimo na chakula (FAO), liliwaleta pamoja viongozi wa ulimwengu kutathmini mbinu bunifu za kuangamiza njaa na kuimarisha utoshelevu wa chakula.

Katika hotuba yake, Mvurya alitaja umuhimu wa kushirikisha  kilimo na ustawi wa viwanda kama suluhu muhimu la changamoto za utoshelevu wa chakula.

Aidha waziri huyo alielezea umuhimu wa kutekelezwa kwa mikakati ya kuimarisha uchumi, kupunguza hasara za baada ya mavuno, kubuni nafasi za ajira na kuimarisha maisha ya watu.

Mvurya alisema jukumu muhimu linalotekelezwa na biashara ndogo na zile za kadri katika kubuni nafasi za ajira, huku akitoa wito wa kupigwa jeki kwa uwekezaji wa biashara ndogo na za kadri.

Alielezea kujitolea kwa Kenya kubuni mifumo thabiti ya utoshelevu wa chakula na kutekelezwa kwa sera na sheria za kuvutia uwekezaji katika mifumo ya chakula kote nchini.

TAGGED:
Share This Article