Mwigizaji Alan Rachins amefariki

Marion Bosire
1 Min Read
Marehemu Alan Rachins

Mwigizaji wa Marekani Alan Rachins amefariki akiwa na umri wa miaka 82.

Mke wake aitwaye Joanna Frank ambaye pia ni mwigizaji aliambia wanahabari kwamba Rachins alifariki akiwa usingizini kutokana na matatizo ya moyo jana Jumamosi alfajiri, saa za Marekani.

Rachins alianza kuigiza miaka ya 1970 wakati alipatiwa majukumu ya uigizaji ya kiwango cha chini kwenye vipindi na hata filamu.

Aliafikia umaarufu mwaka 1986wakati ndugu yake ambaye ni mwandalizi wa vipindi vya runinga kwa jina Steven Bochco, alimpa jukumu la kuigiza kama Douglas Brackman Jr. kwenye kipindi maarufu cha masuala ya sheria “L.A. Law”.

Marehemu aliigiza kwenye sehemu 171 za kipindi hicho cha misimu minane kazi iliyosababisha ateuliwe kuwania tuzo za Golden Globe na Emmy.

Alipata pia fursa ya kuigiza na mke wake Joanna, ambapo waliigiza kama waliokuwa wanandoa awali kabla ya kutengana.

Rachins aliigiza pia kwenye filamu tatanishi ya mwaka 1995 kwa jina “Showgirls” kati ya kazi zake nyingi.

Alan ameacha mke wake wa miaka 46 Joanna na mwanao aitwaye Robert.

Share This Article