Ruto aelekea Bujumbura kuhudhuria kongamano la COMESA

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameondoka nchini mapema leo Alhamisi kuelekea mjini Bujumbra nchini Burundi kuhudhuria Kongamano la 23 la Soko la Pamoja la Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

Akiwa mjini Burundi, Ruto anatarajiwa kuendeleza kampeni ya kumpigia debe Raila Odinga anayegombea uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.

Baadhi ya masuala yatakayojadiliwa kwenye kongamano hilo ni mbinu za kuondoa vikwazo vya kufanya biashara kati ya COMESA na SADC.

Viongozi watakaohudhuria kongamano hilo pia watahudhuria maadhimisho ya miaka 30 tangu kubuniwa kwa COMESA.

Share This Article